Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 SEPTEMBA 2023

08 SEPTEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia habari za masikitiko kuhusu watototo katika migogoro nchini DRC. Pia tunamulika pengo katika usawa wa kijinsia.  Makala tunarejelea ufafanuzi wa ibara ya 9 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu na mashinani tunakuletea ujumbe wa vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

  1. Ukatili dhidi ya watoto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC umepindukia, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo likitolea mfano watoto mapacha ambao hivi karibuni walikutwa wamefungwa mkanda wenye mabomu kiunoni ili yeyote atakayejaribu kuufungua uwezo kulipuka na kusababisha maafa.
  2. Takwimu mpya zilizokusanywa na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa zimeonesha kuwa kuna haja ya uwekezaji wa ziada wa dola bilioni 360 kwa mwaka ili kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake ifikapo 2030.   
  3. Katika makala Anold Kayanda akizungumza na Jebra Kombole, Mwanasheria na Wakili kutoka TAnzania akifafanua Ibara ya 9 ya Tamko la Kimataifa la Haki za binadamu ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75 tangu lipitishwe.
  4. Na mashinani Balozi mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, UNICEF kutoka Uganda ni mmoja wa vijana ambao wanahudhuria Wiki ya Tabianchi ya Afrika nchini Kenya inayokunja jamvi hii leo, wiki iliyoambatana na Mkutano wa Afrika kuhusu tabianchi, uliofunga pazia tarehe 6 mwezi huu wa Septemba nchini Kenya na anatoa ujumbe wa vijana.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'22"