Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 SEPTEMBA 2023

15 SEPTEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea habari kuhusu magonjwa ya mlipuko baada ya majanga, na makaburi ya wafalme wa Uganda. Makala tunakupeleka nchini Tanzania kusikia matarajio wa wananchi tukielekea mkutano wa UNGA78 na mashinani tutasalia hapa hapa Makao Makuu  kusikia ujumbe kuhusu kikao cha ngazi ya juu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kitakachofanyika juma lijalo.  

  1. Kunapotokea majanga au vita na kusababisha watu wengi kupoteza maisha kunakuwa na hofu kuhusu miili ya marehemu kuwa inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa hivyo baadhi ya jamii kwakutokuwa na taarifa sahihi hujikuta wakizika miili hiyo katika makaburi ya halaiki ili kuepuka mlipuko wa magonjwa lakini shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO linasema hiyo si sahihi.
  2. Baada ya kunusurika kwa moto na hatimaye kuwekwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini kuharibika, makaburi ya wafalme wa Buganda huko Kasubi nchini Uganda sasa yako salama na yameondolewa kwenye orodha hiyo baada ya ukarabati uliofanywa na Uganda kwa usaidizi wa Umoja wa Mataifa na wadau.   
  3. Katika makala na wakati macho na masikio ya Dunia yakielekezwa New York Marekani kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaoanza Jumatatu ijayo kujadili mada mbalimbali ikiwemo hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na tunaelekea Tanzania.
  4. Mashinani tutasalia hapa makao Makuu  kusikia ujumbe wa Mwakilishi wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Linda Thomas-Greenfield kuhusu kikao cha ngazi ya juu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kitakachofanyika juma lijalo. 

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
13'23"