Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 JULAI 2022

26 JULAI 2022

Pakua

Hii leo jaridani Anold Kayanda anakuletea Habari kwa Ufupi; Mada Kwa Kina na Mashiani:

Katika Mada kwa Kina anasalia makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako wiki iliyopita Naibu Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Amina J, Mohammed alizindua maonesho ya “Ulikuwa umevaa nini? Yakionesha nguo ambazo walivalia manusura wa ukatili wa kingono, kwa kuzingatia kuwa jamii humbebesha lawama ya kubakwa yule aliyebakwa badala ya aliyebakwa kwa kisingizio cha mavazi.

Habari kwa ufupi ni kuhusu siku ya uhifadhi wa mikoko duniani hii leo na tunakwenda mkoani Pwani nchini Tanzania kusikia harakati za kupanda mikoko. Kisha ni suala la ndui ya nyani na jinsi ya kujitenga pindi mtu akibainika ameambukizwa ugonjwa huo. Na taarifa ya tatu ni mkutano wa FAO wa kuangazia jinsi ya kurutubisha udongo unaotumika kwenye kilimo cha mazao ya chakula.

Mashinani anatamatisha tena na masuala ya mikoko ambako mtaalamu wa mikoko anazungumza. Karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
12'24"