Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 JULAI 2022

19 JULAI 2022

Pakua

Hii leo jaridani tuna mada kwa kina mahsusi ikimulika raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC aitwaye Esperance Tabisha aliyenufaika na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuhamishia wakimbizi nchi ya tatu kupitia mkataba wa kimataifa wa wakmbizi, GCR. Katoka DRC kaingia kambini Kakuma nchini Kenya na kisha Canada na sasa ni mbunifu wa mitindo akitumia mtandao wa kijamii kupata wateja wake. Janga la COVID-19 lilikuwa chungu na tamu hapo hapo kwa vipi? Thelma anasimulia.
Usisahau kuna habari kwa ufupi ikiletwa na Leah Mushi akianza na wakimbizi wa DRC wanaorejea nyumbani kwa hiari kutoka Angola, kisha hatua ya UN kupatia fedha Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ili kukidhi mahitaij ya chakula na mwisho ni watoto kwenye mizozo ikimluika ripoti ya Katibu Mkuu.
Mashinani ni nchini Rwanda ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana Chama cha Madaktari wa Watoto wa nchini Rwanda na Chuo cha Madaktari wa Watoto, Royal College of Pediatrics cha Uingereza ili kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa akina mama na watoto ndani ya siku 1,000 za kwanza za maisha kwa kuimarisha uwezo wa watoa huduma za afya na kwa kuvipa vituo vya afya vifaa muhimu vya matibabu. Noella Uwera ni Muuguzi anayehusika na watoto wachanga katika Hospitali ya Kacyiru katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali. 

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
12'5"