Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 JULAI 2022

22 JULAI 2022

Pakua

Hii leo jaridani kubwa ni kutiwa saini huko Istanbul Uturuki kwa makubaliano baina ya Urusi, Ukraine na Umoja wa Mataifa ya kuwezesha nafaka na vyakula kutoka Ukraine viweze kusafirishwa kupitia Bahari Nyeusi. Shuhuda wa Umoja wa Mataifa kwenye utiaji huo saini si mwingine bali ni Katibu Mkuu mwenyewe wa UN, Antonio Guterres.
Tunakwenda Rwanda kumulika jinsi Mpango wa UN Moja ambapo mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa hushirikiana kutekeleza miradi, huko nchini Rwanda, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linafanya kazi bega kwa bega na mashirika dada likiwemo la Mpango wa Chakula Duniani, WFP na la Chakula na Kilimo, FAO kutekeleza mradi wa Baho Neza au Ishi Vizuri kwa kutumia maafisa ustawi wa jamii wenyeji wanaojitolea. Anold Kayanda ameangazia mradi huo unaoendelea vizuri.
Makala tunakupeleka Beni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mkuu wa kikosi cha 9 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANZBATT-9 kwenye ujumbe wa  ulinzi wa amani wa Umoja huo nchini humo MONUSCO anaeleze jinsi lugha ya Kiswahili inafanikisha lengo lao kuu la ulinzi wa amani. 
Na mashinani utaelekea nchini Tanzania kusikia namna shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani na masuala ya afya ya uzazi, UNFPA linavyosaidia wakunga wataalamu katika kutokomeza ugonjwa wa fistula. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.
 

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
12'59"