Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 JULAI 2022

29 JULAI 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunamulika pengo la huduma za ulinzi kwa wakimbizi na wasaka hifadhi wanapokuwa kwenye safari za kusaka maisha bora.  Ni ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR. Kisha tunabisha hodi Tanzania hususan mkoani Kigoma ambako shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO, limezindua Mtandao wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi TAWFA kupitia mradi wake wa kukuza mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi katika ziwa Tanganyika. Na kwenye makala tunamulika machungu waliyopitia raia wawili wa Ehtiopia katika kusaka uhamiaji MAshariki ya Kati na sasa wamerejea nyumbani kutokana na juhudi za shirika la kazi duniani, ILO na wadau.  Na mashinani shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF limeshauri nchi zote duniani kuongeza uwekezaji katika programu za afya ya akili na ustawi wa familia hususan wakati huu na baada ya janga la COVID-19 kwa kuwa zimeonesha kuleta manufaa zaidi na kupunguza unyanyasaji wa watoto.

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Sauti
13'54"