16 Machi 2022
Hii leo Jaridani Leah Mushi anakuletea sehemu ya pili na ya mwisho ya mahojiano na Jaji wa Mahakama ya Rufaa nchini Kenya, Hannah Okwengu kuhusu manufaa ya jicho la jinsia kwenye mahakama na kile ambacho wamefanikiwa ikiwemo kuanzisha Mahakama ya Familia inayohusika na kesi za ukatili wa kijinsia.