Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 Machi 2022

14 Machi 2022

Pakua

Hii leo jaridani Leah Mushi anakuletea Habari kwa Ufupi zikimulika ufunguzi wa mkutano wa 66 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW66, hali ya chakula Yemen yazidi kudorora na siku ya Hisabati duniani na nafasi yake katika kukabili changamoto za sasa.
Kisha ni mada kwa kina ambayo Assumpta Massoi amezungumza na Jaji Hannah Okwengu wa Mahakama ya RUfaa nchini Kenya kuhusu umuhimu wa jicho la kijinsia kwenye mahakama, hususan uwepo wa majaji wanawake.
Na anatamatisha Jarida na mashinani inayokupeleka Tanzania kwenye soko la hisa la Dar es salaam na harakati zake za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Karibu!
 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
13'12"