Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

3 Machi 2022

3 Machi 2022

Pakua

Jaridani hii leo Leah Mushi anaanzia huko Ukraine ambako mashambulizi yanayoaendelea yanahatarisha afya ya uzazi ya wanawake na watoto wa kike. Kisha anamulika siku  ya kimataifa ya wanyapori akiangazia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kutaka kuendelea kulindwa kwa wanyamapori kwa maslahi ya binadamu na sayari duniani. Suala la uwezeshaji wanawake kiuchumi linamulikwa pia kwa kubisha hodi Kigoma nchini Tanzania ambako Umoja wa Mataifa kupitia FAO unawapa wanawake uwezo wa kujiamini kupitia kilimo cha maharage. Makala ni nchini Afghanistan kumulika changamoto za athari za vita na ukame kwa wanawake wanaoendesha familia na anatamatisha na mashinani ambako mfanyakazi wa kujitolea nchini Poland anahakikisha wakimbizi kutoka Ukraine wanajipatia mahitaji yao ikiwemo yale ya mawasiliano. Karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
13'25"