Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

15 Novemba 2021

Assumpta Massoi anakuletea jarida hii leo ambapo kama livyo ada Jumatatu ni mada kwa kina, tunakupeleka Congo-Brazaville kumulika adha ya kukosa utaifa.

Pia utapata fursa ya kusikia habari kwa ufupi, miongoni mwa utakayosikia ni pamoja na Umoja wa Mataifa watoa fedha kwenye mfuko wake wa dharura kusaidia Ethiopia, WHO wasaidia kupunguzwa bei za vipimo vya haraka vya Kaswende na Virusi vya UKIMWI -VVU, na katika kipindi cha janga la COVID-19 zaidi ya watoto 45,000 waliokuwa wameshikiliwa wameachiliwa huru. 

 

Sauti
11'6"

12 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo Mada yetu kwakina inatokea huko Glasgow Scotland ambapo mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa  mabadiliko ya tabianchi COP26 ukiwa unafunga pazia mwanaharakati wa Mazingira Dkt. Sixbert Mwanga kutoka nchini Tanzania anasema Afrika pamoja na kuwa na kauli moja lakini haijafanikiwa kwenye mkutano huo.

Pia utasikia habari kwa ufupi na kupata fursa ya kujifunza kiswahili .

Sauti
9'56"

11 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo miongoni mwa utakayosikia leo ni pamoja na COVID-19 na bwawa la kienyeji vyarejesha uhai wa kijiji kilichotelekezwa nchini Tunisia.

Kuelekea siku ya kimataifa ya kutokomeza ugonjwa wa Nimonia duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa tiba nafuu UNITAID limetoa wito kwa washirika wote kuongeza kwa kasi ufadhili katika uzalishaji wa oksijeni na kujiunga na ubia wa kampeni ya  KILA PUMZI INAHESABIKA ili kuhamasisha kupunguza vifo vitokanavyo na uchafuzi wa hewa. 

Sauti
12'58"

10 Novemba 2021

Hii leo katika jarida tunakueletea mada kwa kina mahsusi kutoka nchini Tanzania ikiangazia mchango wa vijana na ubunifu wa matumizi ya mifumo ya mawasiliano na teknolojia katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.

Pia utasikia habari kwa ufupi ambao ripoti mbili zimetolewa hii leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa moja ikiangazia masuala ya chakula na nyingine ikiangazia watoto wenye ulemavu duniani.

Sauti
12'20"

09 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo miongoni mwa taarifa utakazo sikia leo ni pamoja na:- 
Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Nepal Sangya Malla anayehudumu katika ujumbe wa Umoja huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo -DRC, MONUSCO ameshinda tuzo ya Afisa Polisi Mwanamke wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2021

Sauti
14'57"

08 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo kama ilivyo ada ya kila Jumatatu tunakuletea mada kwa kina, leo tutakuwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia ziara ya Waambata Jeshi kutoka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC ambao wanaziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa walipozuru wilayani Beni kujionea utendaji kazi wa vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaounda Brigedi ya kujibu mashambulizi FIB MONUSCO.

05 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo ni siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu Tsunami, na kama ilivyo ada leo ni mada kwa kina ambapo tunaangazia vijana na mchango wao katika mabadiliko ya tabianchi wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa COP26 ukiendelea huko Glasgow Scotland. 

Flora Nducha amezungumza na mmoja wa vijana wanaharakati wa mazingira kutoka nchini Kenya na mshindi wa tuzo ya shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP ya champion of the Earth 2020 kutokana na kampuni yake ya Change Makers kubadili taka za platiki kuwa tofali.

Sauti
13'7"

04 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida, leo ni siku ya kimataifa ya kupinga uonevu shuleni na mitandaoni ambapo UNESCO imetaka watoto kulindwa zaidi, WFP imetoa msaada kwa wananchi wa Madagascar wanaoishi katika ukame na hivyo kulazimika kula mmea wa Dungusi kakati.

Pia utasikia kauli ya Rais wa COP26 huko Glasgow kuhusu nchi tajiri kutoa fedha za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
13'18"

3 Novemba 2021

Karibu katika jarida ambapo utasikia kuhusu ushindi wa kijana mtanzania katika tuzo zilizotolewa leo sanjari na mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26.

Habari kwa ufupi leo zimeangazia ripoti ya uchuguzi wa masuala ya haki za binadamu huko Tigray nchini Ethiopia na baa la njaa nchiniMadagascar

Sauti
13'14"

02 Novemba 2021

Leo tarehe 02 Novemba  2021 siku ya kimataifa ya kutokomeza ukwepaji sheria kwa uhalifu dhidi ya wanahabari  ASSUMPTA MASSOI anakuletea jaridi likizungumzia kwa undani juu ya siku hii na takwimu zilizotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni,  UNESCO pamoja na ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.