Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UN News/Ziad Taleb

Mashariki ya Kati bado hali si shwari, UNHCR yapaza sauti

Mashariki ya Kati bado hali si shwari, UNHCR yapaza sauti 

Mapigano huko Mashariki ya Kati yakiingia siku ya tatu kati ya Israel na wapalestina, huko Geneva, hii leo wajumbe wa mkutano wa 54 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu wamesimama kwa dakika moja kuwakumbuka mamia ya watu waliopoteza maisha katika mapigano hayo yaliyoanza baada ya wanamgambo wa Hamas kurusha makombora kuelekea upande wa Israel. Assumpta Massoi na maelezo zaidi. 

(Taarifa ya Assumpta Massoi) 

Nats.. 

Sauti
2'14"
© Unsplash/Omid Armin

Tuzo ya amani ya Nobel yaenda kwa mfungwa Iran, UN yasifu wanawake wa Iran kwa kuongoza vuguvugu

Kamati ya tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu imemtunuku mfungwa mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu wa Iran Narges Mohammadi na Umoja wa Mataifa umepongeza uamuzi huo. Flora Nducha na taarifa zaidi

Baada ya kutangazwa tu leo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imesema “ Kumpatia tuzo Narges Mohammadi mwanaharakati shupavu wa haki za binadamu ambaye hivi sasa anatumikia kifongo cha miaka 16 kwenye gereza la Evin mjini Tehran nchini Iran  kunasisitiza ijasiri na dhamira waliyonayo wanawake wa Iran.”

Audio Duration
2'45"
IMF/Lisa Marie David

Uchumi wa dunia uko njiapanda: UNCTAD

Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD, imezindua leo ripoti yake kuu ya Biashara na Maendeleo ya mwaka 2023 ambayo inachunguza kuimarika kwa uchumi wa dunia na kutoa utabiri wa kinachotarajiwa. Ripoti inaeleza hatua za kisera zinazopaswa kuchukuliwa ili kulinda uchumi wa dunia kutokana na matatizo ya kimfumo ya siku zijazo. 

Sauti
2'58"
UNICEF Ghana

UNICEF yafanikisha mbinu bunifu za ufundishaji na zimeongeza uelewa wa wanafunzi Ghana

Katika kuhakikisha hakuna mtoto yeyote anayeachwa nyuma kupata elimu Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linatekeleza mradi wa kutoa mafunzo kwa walimu nchini Ghana na tayari wanafunzi 37,000 wamenufaika na mafunzo waliopewa walimu wao. Leah Mushi anatuletea taarifa ya Mwalimu Sam mnufaika wa mafunzo yanayofadhiliwa na UNICEF.

Video ya UNICEF inaanza kwa kumuonesha mwalimu Sam anaendesha baiskeli akielekea shuleni

Sauti
1'42"
WHO

Wakimbizi kutoka Kabarakh wasimulia yaliyowasibu

Nchini Armenia, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, linahaha kusaidia wakimbizi wanaoendelea kumiminika nchini humo kutoka eneo la Karabakh linalogombewa kati ya Armenia na Azerbaijan ambako sasa idadi ya wakimbizi waliowasili katika kipindi kisichozidi wiki moja ni zaidi ya laki moja na wako taabani.

Tuko eneo la Goris, jimboni Syunik kusini mwa Armenia, taifa hili la Ulaya Mashariki, wakimbizi wake kwa waume, vijana na watoto wakiwasili kutoka Karabakh, magari yamesheheni virago vyao. 

Sauti
2'1"
UNDP Honduras

Viongozi wa UN wanasema safisha mji wako ili kuunga mkono mzunuko wa uchumi

Mipango ya jamii kudhibiti taka katika maeneo yao inaunga mkono uundaji wa mzunguko wa uchumi, anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya leo ya Kimataifa ya Makazi na anaongeza kuwa “juhudi za umma za kupanua maeneo safi ya kijani yanasaidia kupoza maeneo ya mijini nyakati za mawimbi ya joto.”

Sauti
1'23"
FAO/Giulio Napolitano

FAO waeleza kwa nini kuzuia upotevu na utupaji wa chakula ni muhimu na jukumu la kila mtu

Katika siku ya kimataifa ya uhamasishaji kuhusu uelewa wa Upotevu na utupaji wa chakula, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO linataka kila mtu atambue ni kwanini kuzuia na kupumguza upotevu na utupaji wa chakula ni muhimu hasa katika kuchangia mabadiliko ya mifumo ya chakula na utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs. 

Sauti
2'30"
UNifeed Video

UNMISS wataka wanasiasa Sudan Kusini wapatie wanachi elimu ya kisiasa

Wakati nchi ya Sudan Kusini ikijiandaa kushiriki katika uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza kabisa tangu ipate uhuru, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendesha makongamano na vyama vya siasa nchini humo. 

Ikiwa imesalia miezi 15 mpaka uchaguzi ufanyike hapo Desemba 2024 UNMISS wanasema lengo la kuandaa makongamano hayo nikujenga utamaduni wa kuwa na mazungumzo thabiti, kutatua changamoto zinazowakabili kuhusu utawala bora na kujenga kuaminiana miongoni mwa wanasiasa na jamii wanazozitumikia. 

Sauti
2'21"

28 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wake wamewezesha hatua ya upimaji wa udongo katika wilaya sita ambako mradi wa kulinda na kuhifadhi baiyonuai unatekelezwa. Kazi hiyo imefanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - SUA, na sasa utafiti huo umekamilika, Je umebaini nini? John Kabambala wa redio washirika KidsTime ya Morogoro-Tanzania amehudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo ya vipimo vya udongo.

Audio Duration
11'57"