Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuzo ya amani ya Nobel yaenda kwa mfungwa Iran, UN yasifu wanawake wa Iran kwa kuongoza vuguvugu

Tuzo ya amani ya Nobel yaenda kwa mfungwa Iran, UN yasifu wanawake wa Iran kwa kuongoza vuguvugu

Pakua

Kamati ya tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu imemtunuku mfungwa mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu wa Iran Narges Mohammadi na Umoja wa Mataifa umepongeza uamuzi huo. Flora Nducha na taarifa zaidi

Baada ya kutangazwa tu leo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imesema “ Kumpatia tuzo Narges Mohammadi mwanaharakati shupavu wa haki za binadamu ambaye hivi sasa anatumikia kifongo cha miaka 16 kwenye gereza la Evin mjini Tehran nchini Iran  kunasisitiza ijasiri na dhamira waliyonayo wanawake wa Iran.”

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa ofisi hiyo ya haki za binadamu Liz Throssell amesema “ Nadhani kilicho bayan ani kwamba wanawake wa Iran wamekuwa chanzo cha hamasa ulimwenguni . Tumeshuhudia ujasiri na kujizatiti kwao katika wakati wa ukiukwaji wa haki, vitisho, machafuko na watu kuswekwa vizuizini. Na ujasiri huu na kujizatiti huku ni kwa hali ya juu, kwani wamekuwa wakibughudhwa kwa kile wanachovaa au kutovaa, wanabanwa kisheria, kijamii na kiuchumi kwa hatua zinazochukuliwa dhidi yao.”

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameongeza sauti yake akisema Narges kupewa tuzo hiyo ni kumbusho muhimu kwamba haki za wanawake na wasichana zinakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo kupitia kushitakiwa kwa wanawake watetezi wa haki za binadamu nchini Iran na kwingineko.

Na hivyo “ Tuzo hiyo ya Amani ya Nobel ni “Utambuzi wa wanawake wote ambao wanapambana kwa ajili ya haki za binadamu huku wakihatarisha uhuru wao, afya zao n ahata Maisha yao.”

Narges amefanyakazi kwa miaka mingi kama muandishi wa habari  na pia ni mwandishi wa vitabu na pia naibu mkurugenzi wa shirika la kiraia la Defenders of Human rights Center lililoko mjini Tehran.

MweZi mei mwaka huu alipata tuzo ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari inayotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO

 

Audio Credit
Anold Kayanda/Flora Nducha
Audio Duration
2'45"
Photo Credit
© Unsplash/Omid Armin