28 SEPTEMBA 2023
Pakua
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wake wamewezesha hatua ya upimaji wa udongo katika wilaya sita ambako mradi wa kulinda na kuhifadhi baiyonuai unatekelezwa. Kazi hiyo imefanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - SUA, na sasa utafiti huo umekamilika, Je umebaini nini? John Kabambala wa redio washirika KidsTime ya Morogoro-Tanzania amehudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo ya vipimo vya udongo. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za ulinzi wa amani, haki za binadamu na ubaguzi wa rangi. Na katika kujifunza lugha ya kiswahili tunakuletea maana ya methali “UMEKUWA JETA HUBANDUKI”.
- Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani, Baraza la Usalama limejadili hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo awali Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja huo kuhusu misaada ya kiutu Joyce Msuya anataja changamoto zinazokumba taifa hilo.
- Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk, ametoa wito wa ujumbe wa kimataifa wa kusaidia polisi wa kitaifa nchini Haiti kutokomeza mzunguko wa ghasia uliojikita kwenye ngazi zote za jamii na kuchochea janga la ukosefu wa usalama na haki za binadamu.
- Na mfumo wa kibaguzi dhidi ya wamarekani weusi wenye asili ya Afrika umepenyezwa hadi kwenye utendaji wa jeshi la polisi na mfumo wa mahakama nchini Marekani na hivyo lazima marekebisho ya haraka yafanywe ili kuondokana na madhila yanayokumba wananchi hao, imesema ripoti mpya ya wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.
- Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali “Umekuwa Jeta Hubanduki!”.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'57"