Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UN /Martine Perret)

UNICEF inasema, ebola imeongeza idadi ya watoto waliotenganishwa na wazazi DRC

Watoto zaidi ya 32 wamepoteza au kutenganishwa na mzazi mmoja au wote kutokana na Ebola tangu kuzuka kwa mlipuko mpya Juni Mosi kwenye jimbo la Equateur Magharibi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC,limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Katika taarifa iliyotolewa leo mjini Kinshasa shirika hilo limeonya kwamba hatua za haraka zinahitajika kuongezwa sasa kabla hali hiyo haijageuka kubwa janga kubwa.

Sauti
2'11"
UNOCHA

Guterres: Ulimwengu wa Kiarabu ni wakati wa kugeuza janga la COVID-19 kuwa fursa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameuambia ulimwengu wa nchi za Kiarabu kwamba sasa ni wakati wa kugeuza janga la virusi vya Corona au COVID-19 kuwa fursa ya kujijenga upya na kwa ubora zaidi. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Guterres kupitia taarifa ya kisera kuhusu janga la COVID-19 na jinsi ya kujikwamua vyema katika nchi za ulimwengu aloyoitoa hii leo amesema janga hilo limedhihirisha mapungufu na hali tete katika jamii na uchumi duniani kote na ulimwengu wa Kiarabu haukusalimika.

Sauti
2'30"
UNICEF VIDEO

DRC, mtoto alima bustani kuimarisha lishe na mazingira

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mtoto mwenye umri wa miaka 7 amechukua hatua ya kupanda bustani siyo tu kwa ajili ya kulinda mazingira bali pia kupata mlo pindi familia yake itakapokuwa haina fedha za kununua chakula. Assumpta Massoi anasimulia. 

Mtoto huyo Xavier Kaserka mkazi wa mji wa Goma, jimbo la Kivu Kaskazini anajivunia kuwa mmiliki wa bustani ambapo alipata fursa ya kumtembeza mgeni aliyevutiwa na bustani hiyo.

Sauti
1'45"
UNICEF/ Cherkaoui

Mkimbizi Kaou afaidika na mafunzo ya IFAD kambi ya wakimbizi ya Diffa nchini Niger

Mafunzo ya ujasiriliamali kwa vijana wakimbizi yanayotolewa na mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD kwa msaada wa serikali ya Norway na ushirikiano wa serikali ya Niger kwenye kambi ya wakimbizi ya Diffa nchini Niger, yameleta nuru kwa vijana wakimbizi akiweo Ya Kaou aliyekimbia vita vya Boko Haram nchini Nigeria. Jason Nyakundi anaarifu zaidi.

Sauti
2'13"
IOM/Muse Mohammed

Mmenikirimu nami nalipa fadhila kwa kuwashonea barakoa:Mkimbizi Hamidullah 

Kutana na mkimbizi Hamidullah mwenye umri wa miaka 23. Baada ya kukimbia machafuko Afghanistan na kupokelewa na kukirimiwa na Kijiji cha Pessat-Villeneuve nchini Ufaransa kwa msaada wa shirika la Umoja wa  sasa analipa fadhila kwa kuisaidia jamii inayomuhifadhi kupambana na janga la corona au COVID-19. John Kibego na maelezo zaidi.

Katika Kijiji kidogo cha Pessat-Villeneuve mkimbizi huyu Hamidullah anasaidia mapambano dhidi ya COVID-19 nchini Ufaransa kwa kutumia ujuzi wake wa ufundi cherahani aliourithi toka kwa mama yake. 

Sauti
1'47"
ITC VIDEO

ITC yawezesha wanawake Buhigwe kukamua mawese kwa saa 1 badala ya saa 8

Mradi wa pamoja wa Kigoma, KJP nchini Tanzania unaoendeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa umeendelea kuwa baraka kwa wakazi wa mkoa huo ambapo wanufaika wa hivi karibuni zaidi ni kikundi cha wanawake kata ya Janda wilaya ya Buhigwe, kilichopatiwa kiwanda kidogo cha kuchakata mafuta ya mawese, na hivyo kuondokana na njia ya kienyeji. Assumpta Massoi na maelezo zaidi

Sauti
3'9"
FAO/Rudolf Hahn

Ripoti ya FAO yaonesha dunia imepoteza ekari milioni 178 za misitu tangu 1990

Ripoti mpya ya tathimini ya rasilimali ya misitu iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula FAO imesema upotevu wa misitu duniani bado unaendelea ingawa sio kwa kiwango kikubwa sana. Jason Nyakundi anaarifu zaidi.

Ripoti hiyo mpya ya aina yake iliyozinduliwa leo mjini Roma Italia kwa mujibu wa FAO ni ya kina na imemulika zaidi ya vyanzo 60 vya upotevu wa misitu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1990 hadi 2020.

Sauti
5'49"
UNHCR/Caroline Gluck

Sintosahau nilichokishuhudia kambini Bangladesh:Mkimbizi Asma

Kutana na Asma binti wa miaka 9 mkimbizi kutoka Myanmar ambaye sasa anaishi kwenye kambi ya wakimbizi wa Rohingya ya Katupalong nchini Bangladesh. Anakumbuka alichokishuhudia walipowasili kambini hapo . Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Asma akiwa ndani ya hema yao kwenye kambi ya wakimbizi ya Katupalong Bangladesh anachora picha za safari yake ilivyokuwa kutoka Myanmar mpaka kufika kambini hapo.

Akiwa na umri wa miaka saba tu machafuko yalizuka Myanmar ikabidi yeye na wazazi wake kufingasha virago na kukimbia ili kunusuru maisha yao.

Sauti
1'47"