Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sintosahau nilichokishuhudia kambini Bangladesh:Mkimbizi Asma

Sintosahau nilichokishuhudia kambini Bangladesh:Mkimbizi Asma

Pakua

Kutana na Asma binti wa miaka 9 mkimbizi kutoka Myanmar ambaye sasa anaishi kwenye kambi ya wakimbizi wa Rohingya ya Katupalong nchini Bangladesh. Anakumbuka alichokishuhudia walipowasili kambini hapo . Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Asma akiwa ndani ya hema yao kwenye kambi ya wakimbizi ya Katupalong Bangladesh anachora picha za safari yake ilivyokuwa kutoka Myanmar mpaka kufika kambini hapo.

Akiwa na umri wa miaka saba tu machafuko yalizuka Myanmar ikabidi yeye na wazazi wake kufingasha virago na kukimbia ili kunusuru maisha yao.

Anasema safari ilikuwa ndefu na ngumu iliwachukua siku 9 kuwasili Bangladesh na baada ya familia yake kufika hapo walikumbana na msimu mbaya wa monsoon ambao Asma anasema hatousahau asilani “Niliona mapaa yakiezuliwa, mafuriko na maporomoko ya udongo wakati wa kila mahali. Niliona upepo mkali na hata paa ya nyumba yetu ilibebwa , ikabidi kukarabati tena , niliogopa sana”

Muda mfupi baada ya hapo Asma na familia yake walipewa makazi mapya na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kambini hapa wanapoishi sasa na kumpa faraja na matumaini makubwa Asma na familia yake “Inanipa furaha wakati ambapo hakuna kimbunga. Napenda kwenda kusoma katika vituo vya elimu, na kucheza na marafiki zangu. Najihisi faraja na furaha kuwa hapa Bangladesh.”

UNHCR na wadau wanaendelea kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa Rohingya kama Asma wakati huu ambapo msimu wa Monsoon unaendelea na sasa janga la COVID-19 limeongeza mahitaji hivyo imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada kwa ajili ya wakimbizi hawa.

Audio Credit
Flora Nducha/Jason Nyakundi
Audio Duration
1'47"
Photo Credit
UNHCR/Caroline Gluck