Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IFAD yasaidia maendeleo ya kilimo Senegal

IFAD yasaidia maendeleo ya kilimo Senegal

Pakua

Nchini Senegal, wakulima na wafanyabiashara wadogo wameushukuru mradi wa kusaidia maendeleo ya sekta ya kilimo, PAFA, unaofadhiliwa na Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD. Anold Kayanda na maelezo zaidi. 

(TAARIFA YA ANOLD KAYANDA)

Katika eneo la Niakhar, mkoa wa Fatick nchini Senegal, shughuli za kuvuna mtama zinaendelea kwenye mashamba yanayomilikiwa na chama kijami cha michezo na utamaduni cha Jamm Bugum.  

Kupitia mradi wa kusaidia sekta ya kilimo PAFA, unaofadhiliwa na IFAD, vijana hawa wa Senegal kati ya mwaka 2012 na mwaka huu 2020 wameweza kuongeza uzalishaji kutoka hekta 200 hadi 500 na mavuno yameongezeka.  

Mtama wanouvuna, unaenda kwenye kiwanda chao cha kisasa ambamo wanaoka mikate. Mikate hiyo inasambazwa kwa bei ya jumla kwa wauzaji, ambao wanauza rejareja na wanasema imewakwamua sana kuliko ambavyo wangetumia mchele na sasa kwa kiasi wanaweza kumudu maisha.  

Mama huyu anasema kila siku anaweza kupata faida ya kati ya faranga 3500 hadi 4000 za fedha ya Afrika Magharibi sawa na takribani dola 7 za kimarekani. Anahifadhi fedha zake, anaweza kuzitumia zinapohitajika kwa ajili ya watoto wake, yeye mwenyewe na hata kumsaidia mumewe. 

Profesa Moussa Balde ni Waziri wa kilimo na maendeleo ya jamii, anautambua mchango wa IFAD akisema, “IFAD inafanya jukumu lisilopingika katika maendeleo ya kilimo ya Senegal kwa kushirikiana na taifa la Senegal.” 

 

 

Audio Credit
UN News/Anold Kayanda
Audio Duration
1'30"
Photo Credit
UN News/ John Kibego