Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuteka maji mbali kulinikwamisha kwenye hesabu lakini UNICEF imenikomboa- Elina

Kuteka maji mbali kulinikwamisha kwenye hesabu lakini UNICEF imenikomboa- Elina

Pakua

Nchini Malawi mradi wa kusukuma maji kwa kutumia nishati ya jua au sola uliowezeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF umekuwa mkombozi kwa wanafunzi na jamii zinazozunguka mradi huo uliojengwa katika mkoa wa kati. John Kibego na maelezo zaidi.

Katika mkoa wa kati wilaya ya Dedza nchini Malawi, ukame umekuwa chanzo cha ukosefu wa maji iwe shuleni au nyumbani.

Elina Chikumbutso mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 anasema anapenda hesabu lakini uhaba wa maji umesababisha atumie muda mrefu kusaka maji na hivyo kuchelewa darasani kujifunza.

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Magankula Charles kampandure anathibitisha kuwa ukame wa muda mrefu umeathiri wanafunzi ambao wanatumia muda mrefu kuteka maji iwe ya kunywa au kufanya usafi.

Kilio chao kiliitikiwa na UNICEF ambapo Clara Chindime mtaalamu  wa elimu kwenye shirika hilo anasema,  "tulibaini tatizo la maji katika shule hii. Kwa hiyo tuliona umuhimu wa kusogeza maji karibu na shule ili kupunguza umbali wa watoto kutembea kusaka maji kwa kuwa hali hiyo inaharibu mchakato wao wa masomo. »
Matenki ya maji yalifungwa na nishati ya sola inatumika kusukuma maji hadi kwenye mabomba na hivyo kuleta nuru kwa watoto akiwemo Elina.

Elina anasema, « mfumo mpya wa maji ni mzuri mno na tuna furaha kwa sababu maji yapo ndani ya shule. Hii ina maana kwamba wanafunzi wanaweza sasa kuzingatia zaidi masomo yao.”

Manufaa ya mradi huu si tu kwa wanafunzi bali pia wenyeji wa shule hii ya msingi amnapo Mwalimu Mkuu Kampandure anasema, “uwepo wa mfumo huu wa maji umenufaisha pia jamii jirani na eneo hili kwa sababu wanafika hapa kuteka maji kwa matumizi ya nyumbani.”

Sasa Elina pamoja na kuweza kuzingatia masomo zaidi, hatolazimika tena kuondoka nyumbani mapema na kuchelewa kurudi kwa sababu ya kupoteza muda mrefu kusaka maji,

 

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kibego
Audio Duration
1'54"
Photo Credit
UNICEF Malawi Video capture