Chaguo la Mhariri
Makala Maalum
Wanawake
Kila mwaka ya Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake dunini (CSW) hukutana mwezi Machi kujadili namna ya kukabiliana na ukosefu wa usawa ulioenea, unyanyasaji na ubaguzi wa wanawake unaoendelea kuwakabili duniani kote.
Habari kwa Picha
Uwekezaji kwa wanawake ulivyoleta mabadiliko chanya kwenye jamii mashinani
Maudhui ya siku ya wanawake duniani mwaka huu wa 2024 ni Wekeza kwa Wanawake - Chochea Maendeleo. Maudhui haya tayari yamejidhihirisha wazi kuanzia Afrika, Asia, Mashariki ya Kati, Amerika hadi Ulaya kwani mashirika ya Umoja wa Mataifa yamebeba jukumu la kuchochea kasi ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kupitia wanawake. Habari Picha hii ni kithibitisho.
Habari Nyinginezo
Wanawake
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ukiwa umeingia siku yake ya 5 leo, Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikizungumza na washiriki kutoka mataifa mbalimbali. Leo ni baadhi ya washiriki kutoka Tanzania, vinara wa elimu wanaofadhiliwa na Mfuko wa Malala.
Wanawake
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ukiendelea hapa jijini New York Marekani tunavinjari hadi nchini Kenya kumsikia Hakimu Pamela Achieng ambaye azma yake ya kujikita kwenye masula ya kusimamia haki ilichochewa na swali alilojiuliza yeye mwenye ya kwamba “kama mwanaume anaweza kufanya kazi zinazotambulika hasa za kutetea haki za raia katika mahakama kwanini mwanamke asiweze?”