Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sikufahamu Ureno zaidi ya mchezaji nyota Ronaldo- mhamiaji

Enas Fathallah na familia yake kutoka Syria ambao sasa wanaishi Ureno. Picha: IOM/Video capture

Sikufahamu Ureno zaidi ya mchezaji nyota Ronaldo- mhamiaji

Nchini Syria vita ikiingia mwaka wa saba, wananchi bado wanaendelea kukimbia nchi hiyo ili kusaka hifadhi ugenini. Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba zaidi ya wasyria milioni 7 wamekimbilia ugenini na wanapatiwa hifadhi katika nchi ya tatu. Miongoni mwao ni Enas Fathallah na familia yake ambao sasa wanaishi Ureno, nchi ambayo awali hawakuijua kabisa zaidi ya kufahamu kuwa ndiko anakotoka mwanasoka maarufu duniani, Cristiano Ronaldo. Je yapi haliwasibu? Assumpta Massoi anaangazia kwenye makala hii.