Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Ureno

22 MEI 2023

Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya ukatili wa kijinsia nchini DRC na msaada wa kibinadamu nchini Myanmar.  Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunakupeleka Ureno, kulikoni?  

Sauti
11'41"
Ocean Image Bank/Vincent Knee

Tuilinde bahari ili itulinde- Guterres

Mkutano wa pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Lisbon Ureno ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni lazima kubadili mwelekeo na mwenendo wa shughuli za binadamu kwa bahari la sivyo uchafuzi wa bahari utavuruga  harakati zote za kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Ndivyo alivyokuwa anatamatisha hotuba yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo huko Lisbon kwa lugha ya kiswahili kwenye mkutano huo wa baharí ulioandaliwa kwa pamoja na Kenya na Ureno.

Sauti
2'3"
Nataliia Vladimirova na binti yake Oleksandra au Sasha kwenye umri wa miaka 4 wakiwa mjini Lisbon ,Ureno ambako waliwasili tarehe 14 Machi 2022 wakikimbia vita nchini mwao Ukraine
UN News/Leda Letra.

Ukraine: Hofu yangu ni mume wangu- Nataliia

Nataliia Vladimirova alikimbia nyumbani kwake Kharkiv, Ukraine, siku ya kwanza tu Urusi  ilipovamia nchi yao tarehe 24 mwezi Februari, 2022, akiambatana na binti yake Oleksandra mwenye umri wa miaka 4 pamoja na mama mkwe wake. Wao ni miongoni mwa maelfu ya wakimbizi wa Ukraine waliopata hifadhi ya muda nchini Ureno . Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa huko Ureno, Nataliia al maaruf Natasha, anasimulia simulizi wa yale aliyopitia ikiwemo kugawanyika kwa familia sambamba na kupoteza wengine.