Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSMA yadhamini elimu kwa watu wazima Mali

Wanawake waliojiandikisha katika elimu ya watu wazima nchini CAR. Picha: MINUSMA

MINUSMA yadhamini elimu kwa watu wazima Mali

Mbali na majukumu ya kusimamia amani, usalama na utawala wa sheria nchini Mali, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSMA umeanzisha mpango wa elimu ya kuondoa ujinga wa kutokujua kusoma kwa watu wazima hususan wanawake.

 
Kupitia mtandao wake wa Twitter, MINUSMA imesema mradi huo wa elimu hiyo ya watu wazima unatekelezwa mjini Gao, kwa lengo la kudumisha amani, na pia stahamala miongoni mwa jamii iliyogubikwa na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu.
 
Mradi unatekelezwa kwa lugha ya asili ya Songhai na pia kifaransa ukijikita kuelimisha wanawake mjini Gao.
 
Eneo la mafunzo limejengwa na kwa msaada wa MUNUSMA kwa kushurikiana na serikali ya Mali.
 
Hatua hiyo imeungwa mkono na wananchi wa Mali wakisema utasaidia wananchi hususan wanawake katika kijukwamua na umasikini siku za usoni.