Mali

Baraza la Usalama lalaani kitendo cha viongozi Mali kukamatwa

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali kitendo cha kukamatwa kwa Rais wa mpito wa Mali, Waziri Mkuu na maafisa wengine waandamizi wa serikali hiyo tarehe 24 mwezi huu wa Mei, kitendo kilichofanywa na maafisa wa jeshi la serikali ya Mali.

Walinda amani kutoka Uingereza walioko nchni Mali wapiga doria ya siku 28 Gao

Nchini Mali, kikosi maalum cha Uingereza kinachohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA kimeendesha doria ya siku 28 kutoka mji wa Gao hadi Tassiga jimboni Gao kwa lengo la kulinda raia, katika eneo hilo ambalo limekuwa likishuhudia matukio ya ukosefu wa us

Sauti -
2'6"

Walinda amani wa Uingereza nchini Mali wapiga doria ya siku 28 Gao 

Nchini Mali, kikosi maalum cha Uingereza kinachohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA kimeendesha doria ya siku 28 kutoka mji wa Gao hadi Tassiga jimboni Gao kwa lengo la kulinda raia, katika eneo hilo ambalo limekuwa likishuhudia matukio ya ukosefu wa usalama.

Walinda amani 4 wa UN wauawa Mali, 19 wajeruhiwa, Guterres azungumza

Walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu nchini Mali wameuawa kwenye kambi yao huko Aquelhok jimboni Kidal, huku wengine 19 wamejeruhiwa, kitendo ambacho kimelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Walinda amani hao ni raia wa Chad.

Nchini Vurkina Faso, UNHCR yafanikisha kuwapa hifadhi tena wakimbizi wa Mali waliofurushwa katika kambi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR baada ya kuweka mazingira mazuri ya kurejea kwa wakimbizi wa Mali waliokuwa wa

Sauti -
1'47"

UNHCR yafanikisha kuwapa hifadhi tena wakimbizi wa Mali waliofurushwa katika kambi Burkina Faso 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR baada ya kuweka mazingira mazuri ya kurejea kwa wakimbizi wa Mali waliokuwa wamevikimbia vitisho na mashambulizi katika kambi mbili za nchini Burkina Faso, shirika hilo hivi karibuni liliratibu kuhamishwa kwa wakimbizi wapatao 1,211 kutoka Djibo kwenda kambi ya Goudoubo.

16 MACHI 2021

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo  Grace Kaneiya anakuletea 

Sauti -
12'40"

Mashambulizi dhidi ya walinda amani Mali yanaweza kuwa uhalifu wa kivita

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi dhidi ya walinda amani wa chombo hicho huko nchini Mali yanaweza kuwa  uhalifu wa kivita.
 

Kambi ya walinda amani Mali yashambuliwa, walinda amani 20 wajeruhiwa

Hii leo asubuhi kwa saa za Mali, magharibi wa Afrika, walinda amani wa Umoja wa Mataifa kwenye kikosi cha kuweka utulivu nchini humo, MINUSMA wamedhibiti shambulio dhidi ya kituo chao cha muda cha Kéréna kilichopo maeneo ya Douentza katikati mwa Mali.
 

Hatua mpya za usalama zaruhusu wakimbizi wa Mali kurejea kambini kutoka Burkina Faso

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limewasaidia wakimbizi 3,000 kutoka Mali kurejea kambi ya Goudoubo nchini Burkina Faso miezi tisa baada ya ukosefu wa usalama kuwalazimisha kuhama.