Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saratani yasababisha hasara ya dola bilioni 46

Picha na: IAEA
Programu ya IAEA ya kudhibiti saratani kwa kutumia mionzi katika nchi za kipato cha chini na cha wastani

Saratani yasababisha hasara ya dola bilioni 46

Ripoti mpya kutoka katika kituo  cha kimafaida cha utafiti wa ugonjwa wa saratani duniani,IARC inasema ugonjwa huo imezigharimu nchi zenye uchumi wa kati  ,kiasi cha dola za kimarekani bilioni 46 tangu  mwaka 2012.

Katika ripoti hiyo Dkt Alisona Pearce kutoka IARC amesema  nchi hizo zijulikanazo kama BRICS, ambazo  ni China, Brazil, India, Afrika ya kusini  na Urusi ambazo zina idadi ya asilimia 40 ya watu duniani, zinatumia  gharama kubwa katika utafiti na pia matibabu ya ugonjwa wa  saratani, hivyo kuathiri nguvu kazi  na kusababisha hasara kubwa  katika ukuaji wa uchumi.

Kati ya nchi hizo China peke yake imetumia dola bilioni 28 katika kukabiliana na saratani ya ini, maambukizi ya virusi vya homa ya ini aina ya B  na magonjwa mengine ,Urusi wao ni saratani ya ini na shingo, wakati Brazil, Afrika kusini na India wanakabiliwa na saratani ya ini, mdomo na shingo itokanayo ya matumizi yaliokithiri ya tumbaku.

Mkurugenzi wa IARC Dkt Christopher Wild katika utafiti wa shirika hilo amesema  ili kujuia hasara hiyo kubwa katika ukuwaji wa uchumi lazima nchi za BRICS ziweke katika sera za kitaifazitakazo zingatia udhibiti wa matumizi ya tumbaku, mipango ya chanjo ya awali na pia uchunguzi wa mapema wa saratani.