Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu millioni 2.7 bado wakabiliwa na njaa kali Somalia

Mwanamke Msomalia anampa mtoto maji katika kituo cha Usajili kwa ajili ya Misaada. Picha: OCHA/Giles Clarke

Watu millioni 2.7 bado wakabiliwa na njaa kali Somalia

Msaada wa Kibinadamu

Uzalishaji wa chakula pamoja na vyanzo vya mapato vingi nchini Somalia vinatarajiwa kusalia chini kuliko kawaida  katika maeneo mengi nchini humo.

Uzalishaji wa chakula pamoja na vyanzo vya mapato vingi nchini Somalia vinatarajiwa kusalia chini kuliko kawaida  katika maeneo mengi nchini humo.

Hii ni kutokana  na uhaba mkubwa wa mvua za msimu za Oktoba- Disemba mwaka 2017 katika maeneo mengi ya Somalia huku mvua za msimu wa April hadi Juni  zikitabiriwa nazo kuwa za kiwango cha chini.

Mvua zinazosaidia uzalishaji chakula nchini humo ni za aina mbili  Deyr na Ga. Msimu wa Deyr hutokea katika miezi ya Oktoba hadi Disemba kila mwaka na  ule wa Ga unaanza  Aprili hadi Juni kila mwaka.

Lakini kulingana na matokeo ya uchunguzi wa misimu, licha ya tisho la njaa kupungua, bila ya kuwepo kwa msaada, familia nyingi zitakabiliwa na pengo la chakula.

Uchunguzi huo wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, uliofanywa baada ya msimu wa mvua wa Deyr , ukijumuisha shirika linalochanganua  chakula na lishe  kwa ajili ya Somalia pekee-FSNAU na mtandao unaochunguza alama za awali za kuwepo kwa njaa wa FEWS NET. Mradi umefadhiliwa na  shirika la maendeleo la Marekani la USAID, taasisi za srikali pamoja na washirika wengine.

Somalia sasa inakabiliwa na mvua zilizochini ya wastani  wa  mwaka wa tano mfululilizo .Nao utabiri kutoka  taasisi ya kimataifa ya  utafiti wa hali ya hewa pamoja na jamii IRI unaonyesha kama kuna uwezekano wa mvua za msimu wa Gu  kunyesha kiasi cha asili mia 40 ambacho ni chini ya kawaida na hiyo itathiri  sio tu maji, malisho, mavuno, mifugo lakini pia  bei za vya chakula.

Data za shirika la wakimbizi dunaini la UNHCR zaonyesha kama kuhama kwa watu kutokana na  ukame  kulikofikia kilele chake, katika kipindi cha mwanzo cha mwaka 2017, sasa kumepungua, lakini baadhi ya sehemu za mijini kusini mwa Somalia  zinashuhudia mikingamo ya kibiashara huku sehemu zingine za maeneo ya kaskazini na kati zinaathirika na ukame na hivyo sarafu ya eneo hilo inazidi kutitia na sasa maeneo hayo yameorodheshwa kama yaliyo na mgogoro.