Janga la njaa limeongezeka karibu mara nne katika miaka miwli iliyopita nchini El Salvador, Guatemala, Honduras na Nicaragua na kuwaacha takriban watu milioni 8 katika eneo hilo la Amerika ya Kati wakihitaji msaada mwaka huu wa 2021, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP.
Janga la njaa limeongezeka karibu mara nne katika miaka miwli iliyopita nchini El Salvador, Guatemala, Honduras na Nicaragua na kuwaacha takriban watu milioni 8 katika eneo hilo la Amerika ya Kati wakihitaji msaada mwaka huu wa 2021, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP.
Februari 20 ni maadhimisho ya siku ya haki ya masuala ya kijamii. Lakini tunaendelea na muongo mpya tukiwa na chini ya miaka 10 kufikia lengo la kuwepo usawa wa kijinsia. Kwa bahati mbaya bado tuna safari ndefu kwa kitu kilicho muhimu kama chakula na takribani theluthi mbili ya nchi zote duniani wanawake wako kwenye hatari zaidi ya kufa njaa. Kwa kila suala linalowabagua wanawake hufuata lingine la kuwaweka wanawake karibu na umaskini na njaa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP linasema Sudan Kusini ipo katika hatihati ya baa kubwa la njaa kwani inakabiliwa na viwango vya hali ya juu ya kutokuwa na uhakika wa chakula kuwahi kushuhudiwa tangu taifa hilo changa zaidi duniani kupata uhuru wake yapata miaka 10 ili
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP linasema Sudan Kusini ipo katika hatihati ya baa kubwa la njaa kwani inakabiliwa na viwango vya hali ya juu ya kutokuwa na uhakika wa chakula kuwahi kushuhudiwa tangu taifa hilo changa zaidi duniani kupata uhuru wake yapata miaka 10 iliyopita.
Njaa imeongezeka katika eneo la kusini la Madagascar, mfululizo wa miaka ya ukame inazidisha mateso ya maelfu ya watu, kuharibu mavuno na kuzuia watu kupata chakula, limeeleza shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP.
Nchi ya Afghanistan inakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na uhakika wa chakula huku viwango vya utapiamlo vikifurutu ada kutokana na tishio litokanalo na majanga matatu makubwa ambayo ni vita, corona au
Janga la corona au COVID-19 linabadili hatua zilizopigwa katika maendeleo na kuujaribu msingi wa amani ya kimataifa, lakini pia linatoa fiursa ya kushirikiana kuzisaidia serikali na jamii kujijenga vyema upya umesema mkutano wa kimataifa ulioanza leo kwa njia ya mtandao mjini Roma Italia ukiwaleta pamoja wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, taasisi za fedha za kimataifa, Muungano wa Afrika naserikali za Muungano wa Ulaya.
Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP na serikali ya Nigeria wamezindua programu ya msaada wa chakula na fedha taslimu katika maeneo matatu ya mijini yaani Abuja, Kano na Lagos ambako kote huko ni kitovu cha COVID-19 nchini humo.
Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP linasema hali ya kibinadamu nchini Sudan Kusini inaendelea kuzorota kwa kasi wakati wimbi la njaa likienea katika nchi ambayo ina mgogoro, mvua kubwa na mafuriko ambayo yanavuruga upatikanaji wa chakula kwa watu.