Skip to main content

Wadau waendelea kupinga ukeketaji

Wadau waendelea kupinga ukeketaji

Siku ya Kimataifa ya Kupinga ukeketeaji ikiwa imeadhimishwa mwishoni mwa juma, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York leo kunafanyika matukio kadhaa ya kupigia chepuo utokomezwaji wa mila hiyo potofu.

Miongoni mwa matukio hayo ni mjadala kuhusu namna malengo ya maendeleo endelevu yanavyoweza kufikiwa kwa kupinga kitendo.

Miongoni mwa washiriki ni manusura wa mila hiyo na mwanaharakati Inna Modja kutoka Mali ambaye alikeketwa akiwa na umri wa miaka minne hapa anaeleza kwa nini ni muhimu kutokomeza kitendo hicho.

(SAUTI INNA MODJA)