Skip to main content

Uchumi ni lazima uwafae watu kupitia sera mwafaka za kijamii- Ban

Uchumi ni lazima uwafae watu kupitia sera mwafaka za kijamii- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa kunawiri kwa uchumi pekee hakutoshi kutokomeza umaskini na kuendeleza ufanisi kwa manufaa ya wote. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Ban amesema hayo wakati akihutubia kikao cha Kamisheni ya Maendeleo ya Kijamii, ambacho kimefanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York.

Ban amesema kazi ya kamisheni hiyo itakuwa muhimu sana katika kuhakikisha kuwa ajenda ya maendeleo ya mwaka 2030 haimwachi mtu yeyote nyuma.

(Sauti ya Ban)

“Uzoefu umeonyesha kuwa kunawiri kwa uchumi, hakutoshi kutokomeza umaskini na kuendeleza utajiri unaowafaa wote. Uchumi ni lazima ni lazima uwekwe kuwahudumia watu, kupitia sera mwafaka na jumuishi za kijamii.”