Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kunde kwa chakula endelevu na maendeleo: FAO

Kunde kwa chakula endelevu na maendeleo: FAO

Kunde ni zao muhimu lilaloweza kutumika katika kutekeleza ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu SDGS kwa kukabiliana na njaa na kujenga afya bora, limesema shirika la chakula na kilimo FAO. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

Kwa kuzingatia umuhimu wa kunde katika kuzalisha chakula endelevu,usalama wa chakula na lishe, baraza kuu la Umoja wa Mataifa limetangaza mwaka 2016 kuwa mwaka wa kimataifa wa kunde IYP ambapo FAO kwa kushirikiana na serikali na mashirika itaongoza utekelezaji.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva amesema kauli mbiu ya mwaka 2016 ni mbegu lishe kwa mustakabali endelevu ambapo pia ameelezea umuhimu wa kunde katika maendeleo.

Kunde ina asilimia 25 za protini ambazo ni mara mbili hadi tatu zaidi ya ngano na mchele.