Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania na Australia kushiriki mjadala kuhusu siku ya Radio duniani kwenye UM

Tanzania na Australia kushiriki mjadala kuhusu siku ya Radio duniani kwenye UM

Mratibu wa siku ya radio duniani katika radio ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha amesema katika kuadhimisha siku hiyo shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO kwa kushirikiana na Tanzania na Australia litaendesha mjadala kuhusu namna radio inavyowezesha jinsia hususani wanawake na wasichana.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii Bi Nducha anabainisha kile kitakachojiri mnamo tarehe 13 Februari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

(SAUTI FLORA)

Hata hivyo amesema wasikilizaji wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa watarajie kuelimika kuhusu umuhimu wa radio kupitia makala, taarifa mbalimbali na vipindi kuhusu suala hilo ambavyo amesema vitafanywa kwa ushirikiano na radio washirikika

(SAUTI FLORA)

Mahojiano kwa urefu na mratibu wa siku ya radio duniani yatapatikana katika ukurasa wetu.