Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua ya haraka inahitajika kusitisha machafuko Burundi

Hatua ya haraka inahitajika kusitisha machafuko Burundi

Kuendelea kwa machafuko nchini Burundi kumelifanya baraza la usalama la Umoja wa mataifa kutoa wito wa hatua ya haraka kukomesha umwagikaji wa damu.

Tamko lililotolewa na wajumbe wote 15 wa baraza hilo limesema juhudi za usuluhishi zinatakiwa kuongezwa. Mamia ya watu wameuawa katika miezi kadhaa ya machafuko yalizuka baada ya Rais wa Burundi kutangaza atagombea muhula wa tatu wa uongozi.

Takriban watu 200,000 wamekimbia nyumba zao na kwenda nchi jirani . Baraza limewataka wadau wote kushirikiana kwa karibu na mataifa ya Afrika ya Mashariki kwenye juhudi za upatanishi na kuunga mkono mapendekezo ya Muungano wa Afrika wa mpango wa kulinda Amani.

Ongezeko la machafuko limeongeza hofu ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe, huku Umoja wa mataifa ukionya kuwa kutakuwa na athari kubwa endapo suluhu ya kisiasa haitapatikana haraka.