Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa waeleza wasiwasi baada ya maandamano kukatazwa Kalemie

Umoja wa Mataifa waeleza wasiwasi baada ya maandamano kukatazwa Kalemie

Ofisi ya pamoja ya Haki za Binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC imeelezea wasiwasi wake kufuatia uamuzi wa Kamishna Maalum wa serikali ya DRC kwenye mji wa Kalémie na wilaya ya Tanganyika kupiga marufuku maandamano yote ya raia.Taarifa kamili na  Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Kupitia ujumbe mfupi kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO umemnukuu mkurugenzi wa Ofisi ya Haki za Binadamu nchini DRC, José Maria Aranaz akisema uamuzi huo ni dalili inayotia wasiwasi ya kuzorota kwa demokrasia nchini humo.

Hatua hiyo dhidi ya wilaya ya Tanganyika iliyoko mpakani mwa Tanzania ni ya pili baada ya wilaya ya Lumumbashi kukataza pia maandamano yote.

Katika tangazo hilo la tarehe 17 Disemba, maandamano yoyote hata kwenye maeneo binafsi yamepigwa marufuku hadi uamuzi mwingine utakapotangazwa ikidaiwa kuwa lengo ni kuhakikisha maadhimisho ya mwisho wa mwaka yanafanyika kwa amani.