Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawaziri wa nchi za Kiarabu wakutana Cairo kuhusu makazi na maendeleo ya miji

Mawaziri wa nchi za Kiarabu wakutana Cairo kuhusu makazi na maendeleo ya miji

Mawaziri kutoka nchi 15 za Kiarabu wanakutana jijini Cairo, Misri kujadili kuhusu makazi na maendeleo ya miji.

Akihutubia mkutano huo wa kwanza wa aina yake, Waziri wa Misri wa Makazi, Miundombinu na Jamii za Mijini, Mostafa Madbouly, amesisitiza umuhimu wa mkutano huo akiutaja kama hatua ya kwanza katika kuelekea kufikia maendeleo endelevu, na kupanua mbinu za kukabiliana na changamoto za kikanda za sasa na za siku zijazo.

Mkutano huo unalenga kuendeleza uelewa, kubadilishana mawazo na uzoevu kutoka ukanda wa nchi za Kiarabu na kuwasilisha mbinu bora na kupigia debe ushirikiano wa kikanda.

Unalenga pia kutoa mwongozo katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, hususan lengo namba 11, la kufanya makazi ya binadamu kuwa jumuishi, salama, thabiti na endelevu.