Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yakaribisha amri mpya ya JEM kukomesha kutumikisha watoto jeshini

UNAMID yakaribisha amri mpya ya JEM kukomesha kutumikisha watoto jeshini

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika Darfur, UNAMID, umekaribisha amri iliyotolewa upya ya waasi wa JEM mnamo Septemba 30 ya kupiga marufuku usajili na utumikishaji wa watoto jeshini. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Kwa amri hiyo, uongozi wa JEM umewataka wafuasi wake wote watimize kanuni za kimataifa na viwango viwango wastani vinavyohusika na ulinzi wa watoto, na kutii vipengele vyote vya maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu watoto katika mizozo ya silaha.

Kwa amri hiyo pia, uongozi wa JEM umetoa wito kwa makamanda wake wote mbugani kusambaza kwa upana nakala ya amri hiyo.

Usajili na utumikishaji watoto katika vita ni uhalifu mbaya sana chini ya sheria ya kimataifa na sheria ya Sudan kuhusu watoto yam waka 2010.