Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki na ujenzi wa amani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR

Muziki na ujenzi wa amani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, mzozo baina ya wenyewe kwa wenyewe ulioanza mwishoni mwa mwaka 2012  umesababisha maelfu ya raia kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao.

Harakati za kuleta maelewano zimekuwa zikiendelea kila uchao zikizaa matunda katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo na kwingineko hali ikitwama. Miongoni mwa waliokimbia makwao ni Simplice ambaye anaamua kutumia kipaji chake kuleta maridhiano angalau hata ndani ya kambi wanamoishi ili hatimaye amani hiyo iweze kusambaa.

Je ni kipaji gani hicho? Ungana na Assumpta Massoi katika makala hii.