Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa maendeleo ya Morocco ni lazima iwafidi wote kupata chakula: Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa.

Mpango wa maendeleo ya Morocco ni lazima iwafidi wote kupata chakula: Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa.

Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki ya Chakula, Hilal Elver, amekaribisha mafanikio ya nchi ya Morocco katika kupunguza umaskini uliokithiri na kuondoa njaa kupitia mageuzi muhimu ya kiuchumi na kijamii.

Hata hivyo, Elver ametoa wito kwa mamlaka kufikia maeneo yote, kwa kutoa kipaumbele maalum kwa wale wanaoishi katika maeneo ya vijijini na makundi wanyonge.

Aidha, mtaalamu huyo amesema, Morocco ina malengo mazuri na ya kina, ikiwa ni pamoja na Mpango wa taifa wa Maendeleo, ambao una uwezo wa kuhakikisha usalama wa chakula na lishe kwa kila mtu.

Hata hivyo, Elver amesema kuna tofauti katika utekelezaji wa mipango hiyo katika maeneo kadhaa nchini sawa na pengo la miundombinu muhimu katika usambazaji wa mipango hayo kikamilifu.