Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa WHO waangazia matangazo ya bidhaa zisizo na afya kwa watoto

Mkutano wa WHO waangazia matangazo ya bidhaa zisizo na afya kwa watoto

Huko Amman nchini Jordan kunafanyika mkutano wa siku mbili unaongazia athari za kutokuwepo kwa udhibiti wa utangazaji wa vyakula na vinywaji visivyo na afya kwa watoto vinavyoweza kusababisha utipwatipwa. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Mkutano huo ulioandaliwa na shirika la afya duniani, WHO ukanda wa Mediterania ya Mashariki unafanyika wakati huu ambapo utipwatipwa na unene kupita kiasi unaathiri zaidi ya watoto Milioni 42 duniani kote walio na umri wa chini ya miaka mitano.

Mkurugenzi wa WHO ukanda huo Dokta Ala Alwani amenukuu tafiti za kisayansi zisemazo kuwa watoto wanene kupita kiasi tangu utotoni wako katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo, kisukari na hata saratani watakapokuwa watu wazima na hivyo washiriki wanaangalia jinsi ya udhibiti wa mauzo ya bidhaa hizo kama vile soda na vyakula vipatikanavyo haraka au Fast foods.