Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu laazimia kuongeza uwakilishi kwenye Baraza la Usalama

Baraza Kuu laazimia kuongeza uwakilishi kwenye Baraza la Usalama

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja limepitisha azimio la kufanyia mabadiliko Baraza la Usalama, na kuongeza usawa katika uwakilishi kwenye baraza hilo. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Sauti ya Amina)

Sauti Kutesa....

Ni rais wa kikao cha 69 cha Baraza Kuu, Sam Kutesa, akitangaza matokeo ya kura ya kupitisha azimio la kuongeza usawa kwenye Baraza la Usalama, na wanachama wa Baraza hilo.

Hatua hiyo ya Baraza Kuu imepokelewa kama ufanisi mkubwa wa muhula wa Bwana Kutesa, ambao unamalizika leo na kuhitimishwa kwa kikao cha 69.

Akizungumza kwa niaba ya kundi la nchi 69, zikiwemo nchi za Afrika, Mwakilishi wa Kudumu wa Sierra Leone, Balozi Vandi Chidi Minah amesema

(Sauti ya Balozi Minah)