Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sierra Leone yasherehekea kisa cha mwisho cha Ebola

Sierra Leone yasherehekea kisa cha mwisho cha Ebola

Sierra Leone imethibitisha kisa cha mwisho cha homa kali ya Ebola ikiwa ni hatua kubwa na ya mafanikio katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Manmo Agosti 24 Shirika la afya ulimwenguni WHO limethibitisha kuwa kwa mara ya kwanza hakuna mgonjwa yeyote anayetibiwa homa kali ya Ebola na hakuna kisa kingine nchini humo hatua iliyoibua furaha nchini humo.

Nyimbo na kucheza vilikuwa ni sehemu ya nderemo kutoka kwa wahudumu wa afya wakati wakimtoa katika kituo cha matibabu ya Ebola mfanyabiashara wa mitende Adama Sankou, sherehe ambazo pia zilihudhuriwa na Rais wa taifa hilo Ernest Bai Koroma ambaye alitangaza kuwa ni mwanzo wa mwisho wa Ebola.

Kwa upande wake manusura Bi Sankou amesema amejifunza naman aya kujikinga ikiwamo uzikaji saalama na kuosha mikono huku mwakalishi wa WHO nchini humo Dk Anders Nordström akipongeza taifa hilo kwa hatua muhimu na kuwataka waendelee ilikuhakiiksha hakuna kisa kingine.