Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wafanyika kuunga mkono jukwaa la vijana ukanda wa Maziwa Makuu

Mkutano wafanyika kuunga mkono jukwaa la vijana ukanda wa Maziwa Makuu

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukanda wa Maziwa Makuu, Saïd Djinnit, leo ameitisha mkutano wa wadau wa kikanda kuunga mkono jukwaa la vijana la Kongamano la Kimataifa kuhusu Ukanda wa Maziwa Makluu, ICGLR.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni wawakilishi wa sekritariati ya ICGLR na Wizara ya mambo ya Nje ya Kenya.

Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa ni mchango wa viongozi wa ukanda wa Maziwa Makuu katika kuendeleza masuala ya vijana, sambamba na dhamira ya mkakati wa amani, usalama na ushirikiano.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Bwana Djinnit amesema mkutano huo ni hatua muhimu katika kutimiza ndoto ya pamoja ya kuwawezesha vijana na kuwapa fursa mwafaka ya kuchangia amani, usalama na maendeleo ya kikanda, kama ilivyobainishwa katika mkakati wa amani, usalama na ushirikiano kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.