Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania izingatie amani kuelekea uchaguzi Mkuu: Rodriguez

Tanzania izingatie amani kuelekea uchaguzi Mkuu: Rodriguez

Umoja wa Mataifa umeitaka Tanzania kuhakikisha amani katika mchakato wa ucahguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani unaotarajia kufanyika mwezi Okatoba mwaka huu.

Katika mahojiano na kituo cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez amesema Umoja huo umekuwa ukishiriki katika utaratibu wa uchaguzi nchini Tanzanina hususan kupitia Shirika lake la Mpango wa Maendeleo UNDP na mashirika yake mengine ikiwemo UN Women na la Sayansi, elimu na utamaduni, UNESCO.

Amesema ushirikiano huo umuwezesha mabadiliko ya sera na sheria ili kuhakikisha uharaka wa mabadiliko ya kidemokrasia unaendelezwa ili kufikia viwango vya kimataifa.

Hata hivyo amesema kueleka uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

(SAUTI ALVARO)

“Ni muhimu kwamba wakati tukielekea kampeni na siku ya uchaguzi na hatimaye matangazo ya matokeo ya uchaguzi tuwe na mazingira ya amani, kwamba umma uangalie utaratibu wa uchaguzi na matokeo ya uchaguzi kama ya haki na wazi na kama kiashiria kamili cha matakwa ya watu’’