Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika ina mweleko mzuri katika mabadiliko ya kijamii: Otunnu

Afrika ina mweleko mzuri katika mabadiliko ya kijamii: Otunnu

Kongamano la mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu kuthamini enzi, kutambua zama hizi, na kufikiria mustakabli, umaenza mjini New York ambapo imeelezwa kuwa bara la Afrika liko katika mstari sahihi wa kufikia mabadiliko.

Katika mahojiano na idhaa hii, Ochoro Otunnu, anayewakilisha taasisi ya masuala ya mazingira Green belt movement iliyoasisiwa na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel marehemu Profesa Wangari Mathai, amesema ili mashirika ya kiserikali yashamiri ni lazima jamii za Afrika ziruhusu utawala bora, amani na mtangamano. Kuhusu Afrika akasema.

(SAUTI OTUNNU)

Ameongeza kwamba tofauti za jamii ni fursa ya ustawi kwa amani na maendeleo.