UNICEF yaonya madhila wanaokabiliana watoto Myanmar

3 Agosti 2015

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeonya kuwa watoto nchini Myanmar wanakumbwa na janga mara mbili kutokana na madhila ya mafuriko wanayokabiliana nayo hususani wale wanaoishi maeneo yenye umasikini na yanayoibuka kutoka katika machafuko.

Taarifa ya UNICEF inasema kuwa nchi hiyo imekumbwa na mvua nyingi inayoambatana na upepo kutoka katika tufani iitwayo Komen iliyosababisha maporomoko nchini Bangladesh Julai 30 na kuongeza uharibu zaidi.

Kwa mujibu wa serikali ay Myanmar, watu 36 wamefariki dunia na zaidi ya 200,000 nchini humo ni wahitaji huku serkali hiyo ikitangaza ukanda wa janga la asili katika mikoa minne.

UNICEF kwa kushirikiana na serikali na mashirika mengine yaUmoja wa Mataifa yanahaha kutathimini mahitaji ya dharura na kutoa usaidizi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter