Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matarajio ya ufanisi ni makubwa zaidi Somalia kufuatia kongamano la ubia

Matarajio ya ufanisi ni makubwa zaidi Somalia kufuatia kongamano la ubia

Wadau wa kimataifa wamekaribisha ahadi zilizotolewa wakati wa kongamano la ngazi ya juu la ubia mjini Mogadishu, wakizitaja kama zenye kutia matumaini ya ufanisi zaidi nchini Somalia. Taarifa kamili na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Kongamano hilo lilihudhuriwa na waliwakilishi wa ujumbe wa serikali na mashirika 32 tofauti, ikiwemo Umoja wa Mataifa, IGAD, Muungano wa Ulaya, Ujumbe wa Muungano wa Afrika, AMISOM, Marekani na Uingereza, na hivyo kuwa ndilo kongamano kubwa zaidi la kimataifa kufanyika nchini Somalia baada ya miongo miwili.

Wadau hao wamezipongeza ahadi zilizotolewa, wakisema wanatarajia kuwa zitawezesha mchakato wa uchaguzi wa wazi na jumuishi mwaka 2016, kuimarisha usalama, na kuongeza kasi ya kuleta mabadiliko katika maisha ya watu wa Somalia.

Wamesema wanatambua azimio la Baraza la Usalama nambari 2232 (2015) kuhusu umuhimu wa kutoongeza muda uliowekwa kikatiba wa mamlaka za utawala na ubunge, na kwamba ahadi ya kuanza mashauriano ya kitaifa mara moja ili kuafikia mchakato wa uchaguzi na kubadili mamlaka mwaka 2016 ni hatua muhimu.