Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani yaanza kurejea Burundi, wakimbizi warejea pia: UNHCR

Amani yaanza kurejea Burundi, wakimbizi warejea pia: UNHCR

Kuimarika kwa amani nchini Burundi kumesababisha idadi ya wakimbizi wanaorejea kutoka nchi jirani walikokimbilia kusaka hifadhi kuongezeka katika siku za hivi karibuni,  limesema shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR.

Katika mahojiano na idhaa hii, Mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini  Burundi Abel Mbilinyi, amesema UNHCR imepeleka kikosi maalum mikoani kutathimini marejeo ya wakimbizi na kueleza kile ambacho shirika linafanya kwa sasa.

(SAUTI MBILINYI)

Hata hivyo amesema tathimini ya awali inaonyesha kuwa idadi ya wakimbizi wanaowasili sio kubwa ikilinganishwa na idadi ya waliokimbia kusaka hifadhi wakati wa machafuko kuelekea uchaguzi mkuu nchini Burundi.