Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mitandao ya kijamii ni mtaji kwa maendeleo endelevu: Kirkpatrick

Mitandao ya kijamii ni mtaji kwa maendeleo endelevu: Kirkpatrick

Wingi wa mitandao ya kijamii waweza kutumika katika kupata takwimu za masuala mbalimbali mathalani usalama wa chakula na hata masuala ya maafa.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa inayojishughulisha na masuala ya takwimu Robert Kirkpatrick amesema mitandao ya kijamii inayotumiwa na asilima kubwa za watu kwa sasa kupitia simu za mikononi kama vile twitter ikitumiwa kwa njia bunifu inasaidia katika kupanga mipango ya maendeleo.

Akitolea mfano amesema mfumo huo wa kitekenolojia umetumiak wakati wa mafuriko nchini nchini Mexico na akasema..

(SAUTI ROBERT)

‘‘Kiwango cha watu wanavyotumia fedha kwenye simu za mikononi kinatabiri namna wanavyotumia fedha kwenye chakula. Tuliwezza kubaini rikodi za mamilioni ya kadi za salio za simu na tukatumia kufanya utafiiti wa usalama wa chakula. Tukagundua kuwa kuna uwiano wa asilimia 89 kati ya matumizi ya simu za mikononi na chakula katika kaya.’’