Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi za kisiasa za UM zina mchango mkubwa wa amani na usalama duniani:Ban

Ofisi za kisiasa za UM zina mchango mkubwa wa amani na usalama duniani:Ban

Ofisi za kisiasa za Umoja wa Mataifa zinazofanya kazi kwenye mazingira hatari duniani kote zimethibitisha kuleta tofauti kubwa kwa kuondoa mvutano na hata kuwezesha nchi kuepuka kutumbukia katika migogoro mikubwa. Hiyo ni sehemu ya yaliyomo kwenye ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon  iliyotolewa leo kwa Baraza Kuu ikiangazia historia ya ofisi hizo na mabadiliko yake ya utendaji. Bwana Ban amesema ofisi hizo kama ile yaSomalia, UNSOM na ile yaLibya, UNSMIL  zimekuwa chombo cha lazima katika kuendeleza amani na ulinzi duniani na huendeleza majukumu ya ofisi ya katibu Mkuu.  Kwa sasa Umoja wa Mataifa una ofisi maalum 37 za kisiasa ikijumuisha zilizoko eneo husika kama vile Afrika, Mashariki ya Kati na Asia ya Kati pamoja na wajumbe maalumkamayule wa Maziwa makuu. Hata hivyo Bwana Ban amesema katika mazingira magumu zaidi, mafanikio ya ofisi hizo hutegemea ushiriki thabiti wa pande husika kwenye mchakato wa amani na uwepo wa fursa ya kisiasa na usalama kwa ofisi hizo kufanya kazi. Ametolea mfanoSyriaambako mchakato wa amani unasuasua kutokana na kutokuwepo kwa ushiriki wa dhati wa kimataifa, kikanda na kitaifa. Hata hivyo ameahidi kuendeleza mashauriano na nchi wanachama kuhusu dhima ya ofisi hizo na kutoa wito wa kuungwa mkono ili ziweze kuwa vyombo mahsusi vya kuleta amani na ulinzi wa kudumu duniani.