Mamilioni ya watoto Syria hatarini kufuatia uhaba wa maji na joto kali

10 Julai 2015

Kupungua kwa maji safi na salama ya kunywa wakati wa miezi ya kiangazi nchini Syria kunawaweka watoto katika hatari ya kuambukizwa magonjwa yatokanayo na maji, limeonya Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Syria imeripoti visa 105,886 vya kuhara papo hapo. Kumekuwa pia na kuongezeka kwa kasi kwa visa vya homa ya ini aina ya Hepatitis A, visa 1,700 vikirekodiwa katika wiki moja pekee mnamo mwezi Februari.

Kuongezeka kwa machafuko nchini humo kumesababisha mawimbi mapya ya watu kuhama makwao, na hivyo kuweka shinikizo kubwa kwa mitandao ya huduma za maji na kujisafi, ambayo tayari ni hafifu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter