Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikakati mipya yalenga kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030

Mikakati mipya yalenga kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030

Mikakati mipya ya uwekezaji na kuchukua hatua iliyoidhinishwa na Baraza la Afya Duniani, itazinduliwa na kujadiliwa katika kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo, kuanzia Julai 13 hadi 16, mjini Addis Ababa, Ethiopia, kwa minajili ya kuuongoza ulimwengu katika juhudi za kutokomeza malaria duniani ifikapo mwaka 2030. Mwenzetu Priscilla Lecomte anaripoti kutoka Addis Ababa. Tarifa zaidi na Joseph Msami.

(TAARIFA YA MSAMI)

Mikakati hiyo inatoa mwongozo wa kitaaluma na uwekezaji unaohitajika ili kufikia malengo ya kutokomeza malaria yaliyowekwa katika malengo ya maendeleo endelevu yatakayozinduliwa mwaka huu na Umoja wa Mataifa.

Tangu mwaka 2000, hatua zimepigwa katika kupambana na malaria, na hivyo kupunguza vifo vitokanavyo na malaria kwa asimia 58 na kuzuia zaidi ya vifo milioni 6.2 kati yam waka 2001 na 2015.

Licha ya hatua hizo bado malaria ni sababu na matokeo ya umasikini na kutokuwa na usawa kote duniani.

Malaria imetajwa pia kuwa kizuizi cha maendeleo ya kiuchumi, kuvuruga uhakika wa kuwa na chakula, kuzuia watoto kwenda shule, na kudhoofisha uwezo wa nchi kukabiliana na hatari nyingine za kiafya