Mapigano makali yazuka Malakal Sudan Kusini

29 Juni 2015

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini(UNMISS) umeripoti kuzuka kwa mapigano makali jimboni Malakal kati ya SPLA na vikosi vya upinzani vyenye silaha siku ya jumamosi.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York naibu msemaji wa Katibu Mkuu Farhan Haq amesema mapigano hayo yaliendelea usiku kucha na kusababisha majeruhi.

(SAUTI FARHAN)

‘‘Makombora yalitua karibu na eneo la UNMISS jioni ile na risasi ikapenya katika eneo la ulinzi wa raia nakumjeruhi mtoto mchanga mguuni.’’

Amesema mapambano makali yaliendelea jimboni Malakal hapo jana.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter