Skip to main content

UNRWA kupunguza wafanyakazi kutokana upungufu wa fedha

UNRWA kupunguza wafanyakazi kutokana upungufu wa fedha

Upungufu wa fedha unaolikumba Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestinan(UNRWA) umesababisha shirika hilo kutangaza leo kuwa asilimia 85 ya wafanyakazi 137 wa kimataifa wanaofanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi watapunguzwa katika mchakato wa kupunguza wafanyakazi utakaokamilika mwezi Septemba.

Taarifa ya UNRWA inasema kuwa asilimia 35 ya wafanyakazi 137 wa kimataifa watashuhudia kusitishwa kwa mikataba yao katika majuma manne yajayo huku asilimia 50 ya mikataba yao itasitishwa Septemba 30 bila kuhusishwa.

Hata hivyo UNRWA imesema kuwa itachukua hatua za kupunguza gharama kadri inavyowezekana bila kupunguza huduma kwa wakimbizi.